Skip to main content

Mataifa 100 ziada yakusanyika Norway kutia sahihi Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu ya Mtawanyo ya Klasta

Mataifa 100 ziada yakusanyika Norway kutia sahihi Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu ya Mtawanyo ya Klasta

Leo katika mji wa Oslo, Norway wawakilishi wa kutoka zaidi ya Mataifa 100 wamekusanyika kwenye kikao rasmi, cha siku mbili, kilichoandaliwa makhsusi kuziruhusu nchi wanachama kutia sahihi Mkataba wa Kimataifa wa Kupiga Marufuku Mabomu ya Mtawanyo ya Klasta.

Risala ya KM kwenye mkusanyiko huo wa Oslo uliyahimiza Mataifa yote Wanachama kuridhia, na kuidhinisha, bila kuchelewa Mkataba wa Upigaji Marufuku Mabomu ya Mtawanyo ya Klasta.