Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha Mashitaka wa ICC atoa maelezo maalumu juu ya Darfur kwenye BU

Mwendesha Mashitaka wa ICC atoa maelezo maalumu juu ya Darfur kwenye BU

Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki ya ICC, Luis Moreno-Ocampo amewasilisha kwenye Baraza la Usalama (BU) ripoti ya uchunguzi wa Mahakama juu ya madai ya kuendelezwa vitendo vya uhalifu katika Darfur. ~

Alisema ombi lake la kutaka kuidhinishwe hati ya kumshika Raisi Omar al-Bashir wa Sudan sasa linasailiwa na mahakimu wa ICC, na alilitaka Baraza la Usalama lijiandae vilivyo na taathira zitakzofumka baada ya uamuzi wa majaji wa ICC. Aliitaka "jamii ya kimataifa ifanye kila iwezalo, ijiepushe na hatari ya kuonekana miongoni mwa wale wanaoficha ushahidi dhidi ya mauaji ya halaiki na makosa ya jinai yanayokiuka ubinadamu katika Darfur."