Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizi mapya ya VVU yanaweza kupunguzwa watu wakipimwa mapema, inasema ripoti ya WHO

Maambukizi mapya ya VVU yanaweza kupunguzwa watu wakipimwa mapema, inasema ripoti ya WHO

Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) leo wamechapisha, kwenye jarida maarufu liitwalo The Lancet, ripoti ya matokeo ya utafiti kuhusu taratibu zitakazosaidia kudhibiti bora maambukizo ya UKIMWI ulimwenguni.