Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano Mkuu III kukomesha madhila ya kijinsia dhidi ya watoto na vijana waendelea Rio de Janeiro

Mkutano Mkuu III kukomesha madhila ya kijinsia dhidi ya watoto na vijana waendelea Rio de Janeiro

Mkutano Mkuu wa Tatu Dhidi ya Ukandamizaji wa Kijinsia wa Watoto na Vijana, unaofanyika Rio de Janeiro, Brazil umeingia siku ya pili na utaendelea na mijadala yake hadi Ijumaa, tarehe 28 Novemba. Mkutano huu umeandaliwa bia na Serikali ya Brazil, mamshirika ya kiraia na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF).

CUT:IN: “Well, this congress is, actually, different from the first …

GKOUT: .. responsibility, the role that the private sector can play.”

UN Intvw“Mkutano wa safari hii, unatafautiana na vile vikao viwili

Rio de Janvilivyopita .. kwa namna mbili. Awali, ule mkutano wa

BrazilStockholm (Uswidin) wa 1996 na ule wa Yokohama (Ujapani)

25/11/2008uliojumuika 2001, ililenga majadiliano zaidi kwenye biashara ya unyonyaji wa kijinsia dhidi ya watoto na vijana, waliolazimishwa kushiriki kwenye biashara ya umalaya au filamu za matusi na uchi. Lakini Mkutano wa Rio unazingatia, kwa ujumla, aina zote za unyanyasaji, na ukandamizaji wa kijinsia dhidi ya watoto na vijana. Kwa hivyo, utona wajumbe wa kimataifa wanazungumzia namna ya kutatua klile tatizo la, mathalan, wanajeshi wanaolinda amani wa UM ambao walikutikana wakiendeleza vitendo karaha vyua kunajisi watoto, katika mazingira yanayofufuka kutoka uhasama na mapigano; na pia kuzingatiwa lile suala la baadhi ya viongozi wa kidini waliotuhumiwa kuharibu watoto wadogo, na wawakilishi hawo wanajadilia ile tabia, isio sawa, ya mwalimu kutisha mwanafunzi kwamba hatofaulu mtihani pindi akikataa kujamiana naye, aina ya uhusiano ambao wenye madaraka, au mamlaka, hutumia nguvu ya hadhi yao kukandamiza kijinsiya watoto na vijana, umma ulio dhaifu – hali ambayo inamaanisha madaraka yao yanatumiwa kwa njia mbaya inayotengua imani; haya ndio mambo yanayosailiwa wiki hii kwenye kikao cha Rio de Janeiro kuzingatia hifadhi bora kwa watoto na vijana husika.”