Skip to main content

Mapigano Rutshuri yalazimisha raia kuelekea Uganda kunusuru maisha

Mapigano Rutshuri yalazimisha raia kuelekea Uganda kunusuru maisha

Shirika la UM la Kuhudumia Wahamiaji (UNHCR) limeripoti maelfu ya raia wa eneo la Kivu Kaskazini, katika JKK, wameonekana wakimiminikia kwenye mji wa Ishasha, mipakani Uganda, kujiepusha na mapigano na vurugu liliofumka katika siku za karibuni kwenye maeneo yao, yalioendelezwa na wapiganaji waliochukua silaha.

Francesca Fontanini, msemaji wa UNHCR, alinakiliwa akisema wingi wa wahamiaji wa JKK waliomiminikia Uganda, hivi sasa, walionyesha athari za kupatwa kihoro, hasa baada ya kulazimika kutembea masafa marefu, na kwa siku nyingi, kutafuta hifadhi na usalama katika nchi jirani.

Sikiliza ripoti ziada kwenye idhaa ya mtandao.