Skip to main content

Katibu Mkuu na Baraza la Usalama washutumu mashambulio ya kigaidi Mumbai

Katibu Mkuu na Baraza la Usalama washutumu mashambulio ya kigaidi Mumbai

KM Ban Ki-moon na Baraza la Usalama wameshtumu, na kulaani vikali, mashambulio ya kigaidi yaliofanyika, kuanzia tarehe 26 Novemba, kwenye mji wa Mumbai, Bara Hindi; matukio ambayo yalisababisha watu kadha kuchukuliwa mateka, zaidi ya watu 140 kuuawa na watu 300 ziada kujeruhiwa.