Huduma za WFP Afrika Magharibi zinahatarishwa na ukosefu wa fedha
Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa onyo linalosema huduma muhimu za ndege zinazotumiwa kuwapatia misaada ya kiutu mamia elfu ya watu maskini katika Afrika Magharibi zinahatarishwa kusitishwa, kwa sababu ya ukosefu wa misaada ya fedha kutoka wahisani wa kimataifa.