Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

"Wahamiaji 29 wa Kifalastina wapatiwa makazi mapya Iceland": UNHCR

"Wahamiaji 29 wa Kifalastina wapatiwa makazi mapya Iceland": UNHCR

Wahamiaji wa Falastina karibu darzeni mbili, walionaswa kwa miaka miwili kwenye kambi ya wahamiaji ya Al Waleed, iliopo kwenye eneo la jangwa, mipakani kati ya Iraq na Syria wanatarajiwa kuelekea makazi mapya ya kudumu katika taifa la Iceland, kwa mujibu wa Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR).

Kundi hilo linajumuisha watu walio dahiifu, hasa wahamiaji watoto na wanawake, ambao baadhi yao walipoteza waume zao kutokana na fujo na vurugu la Iraq. Kwa kulingana na hali hiyo UNHCR inaamini nafasi iliosalia ya kuwanusuru wahamiaji hawa kimaisha ni kuwapeleka uhamishoni katika maeneo mapya ambapo watapatiwa makazi ya kudumu.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.