Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Wajumbe wa kudumu wa Uchina na Urusi katika Baraza la Usalama wamepiga kura ya turufu, au kura ya veto, kupinga lile azimio liliodhaminiwa na Marekani na baadhi ya nchi, la kuweka vikwazo dhidi ya Zimbabwe, ikijumuisha uamuzi wa kupiga marufuku kusafiri na kudhibiti mali za Raisi Robert Mugabe pamoja na utajiri wa viongozi wengine kumi na mbili wa Zimbabwe. Mswada wa azimio ulipigiwa kura tisa za upendeleo, ikijumuisha Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji, Burkina Faso, Costa Rica, Croatia, Utaliana na Panama wakati Indonesia kutopiga kura. Mataifa yaliounga mkono Uchina na Urusi kwenye kura ya upinzani yalijumuisha Afrika Kusini, Libya na Vietnam.

Halkadhalika, Baraza la Usalama Alkhamisi limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kuondosha vikwazo vya silaha dhidi ya Rwanda na vile vile kusitisha Kamati ya Vikwazo kwa Rwanda.

KM Ban Ki-moon na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Pakistan, Makhdoom Shah Mahmud wamefikia mafahamiano maalumu Alkhamisi baada ya mkutano wao kuzingatia uwezekano wa UM kuisaidia Pakistan kuendeleza uchunguzi kuhusu mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Marehemu Benazir Bhutto.