Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU inazingatia ripoti ya Katibu Mkuu juu ya UNAMID

BU inazingatia ripoti ya Katibu Mkuu juu ya UNAMID

Baraza la Usalama limekutana asubuhi kushauriana juu ya ripoti mpya ya KM kuhusu operesheni za vikosi mseto vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID). Kuna ripoti ya kwamba Uingereza inajaribu kulishawishi Baraza la Usalama kutoa taarifa kali itakayotuhumu mashambulio ya wiki iliopita kwenye kambi za vikosi vya UNAMID Darfur kuwa ni makosa ya jinai ya vita, ambapo darzeni ya walinzi amani ama waliuawa au kujeruhiwa.