Wajumbe wa Kenya watathminia Mkutano wa Kimataifa juu ya UKIMWI
Mkutano wa Hadhi ya Juu wa Baraza Kuu Kuzingatia Masauala ya Kudhibiti Bora UKIMWI uliochukua siku tatu umekamilisha mijadala yake Alkhamisi magharibi, ambapo kabla ya kufunga kikao Raisi wa Baraza Kuu Srgjan Kerim aliyahimiza Mataifa Wanachama kuendelea kuimarisha mafanikio yao muhimu ya kupanua uwezo wa umma kupatiwa huduma kinga dhidi ya UKIMWI, pamoja na misaada ya matibabu kwa wale raia walioambukizwa na VVU itakapofika 2010.~~
Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM ilifanya mahojiano na wawakilishi wawili wa kutoka Kenya, akiwemo mwakilishi wa Serikali, Dktr Naomi Shaban, aliye Waziri wa Mipango Maalumu wa Kenya pamoja na Jemimah Nindo A, mjumbe aliyewakilisha shirika lisio la kiserekali la Mtandao wa Walimu Waliopatwa na VVU Kenya au kwa ufupi Shirika la KENEPOTE.
Sikiliza tathmini yao juu ya mkutano kwenye idhaa ya mtandao.