Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame uliokithiri Ethiopia wailazimisha OCHA kuomba msaada ziada

Ukame uliokithiri Ethiopia wailazimisha OCHA kuomba msaada ziada

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ikijumuika na mashirika mengine ya UM na Serikali ya Ethiopia, yameripoti kwamba wamelazimika kuomba waongezewe misaada ya dharura na wahisani wa kimataifa kwa sababu ya kujiri kwa hali mbaya ya ukame Ethiopia. Msaada huo unatakiwa kuwahudumia chakula mamilioni ya waathiriwa wa ukame ambao idadi yao katika siku za karibuni ilikithiri kwa kiwango kikubwa kabisa.