Skip to main content

BU limepitisha azimio la kuisadia Usomali kupata amani

BU limepitisha azimio la kuisadia Usomali kupata amani

Baraza la Usalama (BU) limepitisha Alkhamisi, kwa kauli moja, azimio muhimu juu ya Usomali, azimio nambari 1814 (2008) ambalo lilimtaka KM Ban Ki-moon kuendelea na matayarisho ya ule mradi wa msingi, utakaotumiwa kuchangisha huduma za kihali na mali kutoka jumuiya ya kimataifa, ili kusaidia kurudisha tena usalama na amani nchini Usomali.