Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM anasisitiza usalama Afrika ya Kati unaregarega, lakini kuna matumaini

KM anasisitiza usalama Afrika ya Kati unaregarega, lakini kuna matumaini

Sergio Duarte, Mjumbe Mkuu wa Masuala ya Upunguzaji wa Silaha jana Alkhamisi alihudhuria mkutano wa Kamati ya Ushauri juu ya Masuala ya Usalama katika Afrika ya Kati uliofanyika Luanda, Angola. Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo kwamba juhudi za kimataifa za karibuni, za amani, zilifanikiwa, kwa kiwango wastani, katika kurudisha imani ya kutia moyo juu ya matumaini ya kufufua tena usalama na amani kwenye eneo hilo.

Duarte aliyasema hayo kwa niaba ya KM. Alitoa mfano wa matumaini anayobashiria ambapo kulipatikana mafanikio kwenye majadiliano yaliohusu mvutano uliojiri katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kadhalika, alitupa mfano mwengine unaoelezea mafanikio yaliopatikana kwenye mkutano wa Goma uliosailia uwezekano wa kurudisha tena, kwa polepole, amani katika Jimbo la Kivu; na pia alikumbusha kwamba vikosi vya ulinzi wa amani vya UM vya MINURCAT vimeshaenezwa katika sehemu kadha wa kadha za kaskazini-mashariki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad mashariki.