Skip to main content

UM umechukizwa na mauaji katili Darfur ya ofisa wa UNAMID

UM umechukizwa na mauaji katili Darfur ya ofisa wa UNAMID

UM umepokea taarifa zenye kusema ofisa mmoja wa vikosi mseto vya UM na UA katika Darfur, au vikosi vya UNAMID, aliotokea Uganda alikutikana Ijumatano magharibi ameuawa, ndani ya gari ya kazini, ilioegezwa karibu na marikiti ya mji wa El Fasher, Darfur kaskazini, kwa mujibu wa Msemaji wa UNAMID, Noureddine Mezni. Marehemu huyo, Inspekta John Kennedy Okecha tuliarifiwa alipigwa risasi tatu - shingoni, kifuani na kwenye tumbo.