Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa Afrika Mashariki kwenye UNCTAD XII asailia kikao

Mjumbe wa Afrika Mashariki kwenye UNCTAD XII asailia kikao

Wajumbe kadha kutoka Mataifa Wanachama wa UM walikusanyika katika mji mkuu wa Accra, Ghana kuhudhuria kikao cha 12 cha Taasisi ya UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) ambacho kilifunguliwa rasmi Aprili 20, na mijadiliano yaliendelea karibu wiki moja. Mkutano Mkuu wa UNCTAD hufanyika kila baada ya miaka minne. Dhamira ya kikao cha mwaka huu cha 12 ilikuwa kuzingatia taathira zinazoletwa na huduma za msawazisho wa lazima wa shughuli za uchumi katika soko la kimataifa, au kwa lugha nyengine kuzingatia taathira ya marekibisho yaliochochewa na mfumo wa utandawazi.

Alkhamisi Mwandishi habari wa Redio ya UM, Maoqi Li alipata fursa ya kumhoji Marco James Kassaja, mjumbe wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania uliopo Geneva. Mwandishi wetu alimuuliza Mjumbe Kassaja kwa nini mvutano umekithiri katika hekaheka za kufikia maafikiano ya kuridhisha, mnamo saa za mwisho za majadiliano kabla ya kikao cha UNCTAD kumalizika.

Sikiliza jawabu kwenye idhaa ya mtandao.