Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fafanuzi za Mjumbe wa Afrika Mashariki kuhusu kikao cha mwaka cha CSW

Fafanuzi za Mjumbe wa Afrika Mashariki kuhusu kikao cha mwaka cha CSW

Kamisheni ya UM juu ya Haki ya Wanawake Duniani (CSW)ilikusanyisha wajumbe kadha wa kadha wa kimataifa, kwenye Makao Makuu ya UM, waliohudhuria kikao cha mwaka, cha 52, ambapo kuanzia tarehe 25 Februari hadi Machi 07, 2008 wajumbe hawa walizingatia kipamoja yale masuala yanayohusu haki za wanawake.

Miongoni mwa wajumbe wa kutoka Afrika Mashariki waliohudhuria kikao cha mwaka huu cha Kamisheni ya UM juu ya Haki za Wanawake (CSW) alikuwemo Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto kutoka Zanzibar, Tanzania, Asha Abdullah Juma. Nilipata fursa ya kufanya mahojiano naye kwenye studio za Redio ya UM ambapo alitupatia maoni yake halisi juu yamkutano na matarajio aliyoanayo kwa siku za usono juu ya haki za kijinsia.

Sikiliza maelezo kamili kwenye idhaa ya mtandao.