Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa KM anasema mwafaka wa Uganda na waasi unaashiria matumaini mema

Mjumbe wa KM anasema mwafaka wa Uganda na waasi unaashiria matumaini mema

Raisi mstaafu wa Msumbiji, Joaqim Chissano, ambaye ni Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Tatizo la waasi wa LRA Uganda alianza ziara ya upatanishi Uganda Ijumaa iliopita. Baada ya hapo Chissano alielekea Juba, Sudan Kusini kuendelea na mazuungumzo ya upatanishi baina ya Serikali ya Uganda na waasi wa LRA. Msuluhishi Dktr. Riek Machar Dhurgon Teny, aliye naibu-raisi wa Serikali ya Sudan Kusini naye pia amejumuika kwenye majadiliano hayo.~~

Raisi Chissano alihadharisha kwamba licha ya kuwepo ishara hizo za kutia moyo juu ya suluhu ya mvutano ulioselelea kitambo kati ya Serikali ya Uganda na waasi wa LRA, hana hakika kama jedwali ya mazungumzio yao itawaruhusu kukamilisha mapatano kabla au baada ya mwisho wa mwezi Februari.