Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ameingiwa wasiwasi kurejewa kwa mapigano Darfur Magharibi

KM ameingiwa wasiwasi kurejewa kwa mapigano Darfur Magharibi

KM Ban Ki-moon ameripoti, kwa kupitia msemaji wake, kuingiwa na wasiwasi mkubwa juu ya kurejea tena kwa mapigano, katika eneo la Darfur Magharibi la Aro Sharow, baada ya kambi ya wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) iliposhambuliwa kwa mabomu kwa siku mbili mfululizo, katika tarehe 18 na 19 Februari.

Tukio hili, alisema KM ni kitendo kisichokubalika hata kidogo na jamii ya kimataifa. KM Ban alipendekeza kwa makundi yote husika na mzozo wa Darfur kusitisha, halan, uhasama kati yao na kujaribu kushiriki kikamilifu kwenye ule utaratibu ulioandaliwa na kuongozwa na wapatanishi wa UM na UA kwa Darfur, wa kurudisha tena utulivu na amani kwenye eneo lao. Alikumbusha na kunasihi kwamba ni vigumu kwa mapatano ya amani kufanikiwa katika mazingira yaliojaa uhasama na vurugu,hali ambayo huwalazimisha raia kuhama makwao kidharura ili kunusuru maisha.