Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUC inasaidia kuandaa usalama DRC kwa mkutano wa upatanishi

MONUC inasaidia kuandaa usalama DRC kwa mkutano wa upatanishi

Shirika la UM linalosimamia ulinzi wa amani katika JKK (MONUC) limearipoti kwamba linaisaidia Serikali ya taifa kuandaa mazingira ya usalama, kuambatana na mkutano utakaofanyika tarehe 6 Januari (2008) kwenye Jimbo la Goma, katika eneo la mashariki kuzingatia suluhu ya upatanishi na masuala ya kusukuma mbele shughuli za maendeleo katika eneo la mapigano.

Wiki iliopita ndege za MONUC zilifanikiwa kusafirisha batalioni kadha za wanajeshi wa taifa wa FARDC, waliopelekwa Kivu Kaskazini kuchunga usalama na kuhakikisha mkutano utafanyika kwa amani na bila ya fujo. Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba mchanganyiko wa mazingira ya uhasama pamoja na ongezeko la kijeshi, na uvunjaji sheria Kivu Kaskazini ni mambo yaliyochochea na kuwalazimisha watu 400,000 kuhajiri makwao katika 2007. Ama jumla ya watu waliong'olewa makazi tangu 2003 kutokana na mapigano inakadiriwa na UNHCR kufikia 800,000.