Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani humaanisha nini katika 2007?

Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani humaanisha nini katika 2007?

Tarehe mosi Disemba huadhimishwa kila mwaka na Mataifa Wanachama, kuwa ni Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani ambapo walimwengu hukumbushana juu ya jukumu linalowasubiri kukabiliana na janga hili hatari la afya. Taadhima za mwaka huu zimetilia mkazo zaidi umuhimu wa kuwa na ‘uongozi bora’ katika kukamilisha ahadi za kuutokomeza UKIMWI ulimwenguni.

Hivi majuzi Idara ya Habari ya UM (DPI) pamoja na mashirika yasio ya kiserekali (NGOs) yaliandaa kikao maalumu kwenye Makao Makuu ya UM, mjini New York kuzingatia masuala ya UKIMWI. Mkutano uliitishwa kwa kulingana na Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani. Mada ya maadhimisho ya mwaka huu ilitilia mkazo umuhimu wa kuwa na uongozi bora katika huduma zote za kukabiliana na matatizo ya UKIMWI duniani. Miongoni mwa viongozi walioshiriki kwenye taadhima za Makao Makuu alikuwemo Daktari Jessie Mbwambo, wa Taasisi ya Magonjwa ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliopo Dar es Salaaam, Tanzania. Nilipata fursa ya kuwa na mahojiano naye kwenye studio za Redio ya UM.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.