Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tathmini ya Mzozo wa Chakula Duniani (I)

Tathmini ya Mzozo wa Chakula Duniani (I)

Hivi karibuni, Idara ya Redio ya UM imetayarisha mfululizo wa vipindi maalumu kuzingatia mzozo wa chakula uliojiri duniani sasa hivi, vipindi ambavyo vimeandaliwa bia na wanahabari wa Idhaa ya Redio ya UM. Dhamira ya vipindi hivi hasa ni kukupatieni taswira halisi ya hali ilivyo kwa kuelezea namna umma wa kimataifa unavyojitahidi kukabiliana na maafa yanayozushwa na mzozo wa chakula kidharura. Tutazingatia suluhu za wastani na zile za muda mrefu zinazotakiwa kufuatwa na mataifa husika kujivua na maafa hayo.

Makala ya awali ya vipindi hivi maalumu inasailia fursa na hatari zilizodhihiri kimataifa kutokana na mgogoro wa chakula duniani. Inatathminia tatizo la kupanda kwa kasi kwa bei za chakula ulimwenguni linavyoathiri idadi kubwa ya watu, hasa katika nchi masikini. Tutagusia sababu zilizozusha ghasia na fujo katika sehemu kadha wa kadha za dunia na mchango wa WFP katika kudhibiti bora mgogoro huo wa chakula kimataifa.

Sikili ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.