Tathmini ya Mzozo wa Chakula Duniani (II)
Bei ya mafuta ya petroli, katika jiji la New York, Marekani na pia kwenye sehemu nyengine za dunia, hasa katika miezi ya karibuni, ilisajiliwa na wataalamu wa kiuchumi kupanda mara kadha, kwa kasi ambayo iliwasumbua watumiaji wingi wa nishati hiyo, na baadhi yao hata walishindwa kumudu kutumia magari yao na kulazimika kutumia vyombo vya usafiri wa umma wa kawaida. Kufuatana na kadhia hiyo ilidhihiri wazi kwamba mahitaji ya nishati – hasa mafuta ya petroli - nayo pia yaliendelea kukithiri ulimwenguni kwa kiwango kikubwa.
Makala ya pili ya mfululizo wa vipindi maalumu juu ya mzozo wa chakula duniani, vilivyotayarishwa makhsusi na wanahabari wa Redio ya UM, itasailia, kwa kina, fungamano zilizopo baina ya kupanda kwa kasi kwa bei za chakula na mfumo wa aina ya kilimo kinachotumia nishati na viumbehai kuzalisha nishati.
Sikiliza kipindi kamili kwenye idhaa ya mtandao.