Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

'Haki za binadamu ni za kila mtu', wakumbusha viongozi wa kimataifa

'Haki za binadamu ni za kila mtu', wakumbusha viongozi wa kimataifa

Umma wa kimataifa kila mwaka huiadhimisha tarehe 10 Disemba kuwa ni ‘Siku Kuu ya Haki za Binadamu Duniani’. Siku Kuu hii ilianzishwa rasmi kimataifa baada ya Baraza Kuu kupitisha, mnamo tarehe 10 Disemba 1948, tamko linalojulikana kwa umaarufu kama Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu.

Tukio hili liliwasilisha hatua ya kihistoria iliothibitish kuwepo ridhaa ya Mataifa Wanachama yaliopendekeza kuanzisha chombo kipya kitakachotumiwa kama kanuni za marejeleo, zitakazosaidia kuongoza mataifa kwenye zile juhudi za kuutekelezea umma haki za binadamu.

Taadhima za mwaka 2007 zinafuatana na juhudi za UM kuanzisha kampeni ya mwaka mzima, itakayotumiwa kuamsha hisia za umma wa kimataifa juu ya umuhimu na ulazima wa kuimarisha haki za binadamu kote ulimwenguni. Kampeni hii itakamilishwa mnamo tarehe 10 Disemba 2008, pale Azimio la UM juu ya Haki za Binadamu litakapotimia miaka 60 tangu kupitishwa.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao, taarifa ambayo inajumuisha, vuile vile mahojiano na mwanaharakati wa haki binadamu wa Afrika Mashariki.