KM ana wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa raia Kivu Kaskazini
KM wa UM Ban Ki-moon ameripoti kuingiwa wasiwasi mkuu juu ya athari kwa raia kutokana na uharibifu wa hali ya utullivu Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Taarifa alizopokea KM zilionesha kukithiri kwa mateso dhidi ya umma raia, ambapo watu huwa wanafukuzwa makwao na unyanyasaji wa kijinsia kuongezeka. Hali hii ilisababishwa na mapigano KivuKaskazini kati ya vikosi vya Serikali na makundi ya wanamgambo na wanajeshi waasi, wafuasi wa Jenrali mtoro Laurent Nkunda.~~
UM na washirika wenzi wanajitahidi kufanya kila wawezalo kuwapatia raia walionaswa kwenye mapigano misaada ya kiutu. Lakini kwa sababu ya ukosefu wa usalama kieneo mashirika yanayohudumia misaada ya kihali hushindwa kukidhia mahitaji ya raia husika.