Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Afrika

Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Afrika

Mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Afrika AU, ulifanyika Accra, Ghana mapema mwezi wa Julai, suala kuu lilikua juu ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa ya Afrika chini ya serekali moja kuu. Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Asha-Rose Migiro aliwahutubia viongozi na kusema kuna changamoto chungu nzima kufikia lengo hilo. ~

Migiro:Hali ya Amani na usalama barani Afrika ni nzuri. Yani hiyo ni nafuu zaidi ukilinganisha na miaka mitatu au mine iliyopita. Nilipata fursa ya kuzungumza na viongozi kadhaa wa Afrika na wameeleza kuridhika na hali huko Sierra Leone. Kuna utulivu huko Ivory Coast, pamoja na Liberia. Kwa hivyo, kwa ujumla kuna maendeleo katika fani ya amani na usalama. Llakini amesema kuna wasi wasi katika baadhi ya maeneo, kwa mfano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Kuna ghasia Kivu ya Kaskazini. Tulizungumza juu ya jinsi AU na UM tunavyo weza kufanya kazi pamoja kutanzua matatizo hayo.

Akizungumzia suala la kuundwa Umoja wa Mataifa ya Afrika alisema, Umoja wa Mataifa unaunga mkono wazo hilo, lakini kuna hitaji kuimarishwa Jumwia za kikanda kwanza.

Migiro: Msimamo wa umoja wa mataifa ni kwamba tunaunga mkono juhudi zote kuelekea umoja wa Afrika kuelekea mungano zaidi ya kanda mbali mbali. Kwa hivyo tunafuatilia mjadala na hatimae tutaona kile wakuu wataifa na serekali watakavyo amaua kufanya, hayo yote yanafuatana na msimamo wa Umoja wa Mataifa kusaidia juhudi zote za Umoja wa Afrika kwa sababu nina dhani hiyo itaiwezesha Afrika kupata nafasi ya kukabiliana na changa moto katika fani za usalama na amani, katika fani za maendeleo.

Bi Migiro amesema kufikia wazo hilo itabidi kukabiliana na changa moto hizo.

Migiro: Baadhi ya changa moto hizo ni matatizo yale yale yanayo ya kumba serekali za nchi za Kiafrika. Kuna masuala ya utawala bora, suala la demokrasia, suala la haki za binadam, masuala maalum yanayohusiana na wanawake na watoto. Hayo yote yanaweza kuwa vipingamizi kwa sababu kuna mataifa yaliyoendelea zaidi na yale ambayo hayajaendelea. Kwa hivyo hizo ndizo changa moto za muungano wa Afrika.

Amesema matatizo makubwa zaidi ni janga la HIV na Ukimwi, pamoja na kuwepo hali ya idadi kubwa ya vifo vya watoto wachanga na kina mama waja wazito.

Migiro: Mambo haya yote yanadhuru juhudi za maendeleo za Africa. Kwa hivyo inabidi wabuni njia za pamoja kukabiliana na matatizo hayo. Hivyo kwa vile wanazungumzia muungano, hiyo ina maana watalazimika kukabiliana na suala hili kama utaratibu wa maendeleo. Kuna kipingamizi kufikia umoja lakini pia kuna kipingamizi kwa maendeleo.

Maendeleo hayo anaema yana ambatana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia, MDG.

Migiro: Malengo haya yalipitishwa na viongozi wa nchi mbali mbali kama ndio dira ya maendeleo. Kuna mambo yanayohusu masuala ua Ukimwi na virusi vya HIV. Kuna kupunguza vifo vya watoto wachanga na kina mama waja wazito. Lakini kuna suala zima la kupunguza umaskini na tunafikiri kwamba serekali ambayo ni imara itawajibika vizuri zaidi kwa wananchi wake na itaweza kushughulikia masuala ya manedeleo.

Anasema wanawake na watoto hawana uwezo wa kwenda katika mazahanati au hata hospitali. Na vile vile kuna tatizo la lishe bora, yote hayo yanahusiana na lengo la kwanza la MDG la kupambana na umaskini. Umaskini unawaweka waafrika katika mviringo usokwisha. Unabaki maskini anasema, huwezi kupata huduma za jamii na huduma zilizopo ni wachache wanaoweza kupata, hivyo wanabaki pale pale, maskini. Hivyo, kufuatana na utafiti, Afrika inaendelea kubaki nyuma na hakuna dalili bara hilo litaweza kutekeleza malengo hayo ifikapo 2005. Hivyo Bi Migiro anasema katibu mkuu ameteua tume maalum kutathmini jinsi utaratibu wa MDG utaweza kuimarishwa zaidi.

Migiro: Lakini, katika baadhi ya mataifa kumepatikana maendeleo katika baadhi ya malengo. Kama nilivyo sema katika hotuba yangu kwenyekwa mkutano wa viongozi wa AU, kuna maendeleo mazuri kama kuandikishwa watoto shule huko Ghana, Kenya, Tanzania na Uganda. Nayo malaria inadhibitiwa huko Niger, Togo na Zambia na kuna maeneo mengine ya maji na usafi. Kwa hivyo utaona kuna maendeleo ya hapa na pale hiyo haitoshi.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alihadi kuendelea kwa msaada wa UM kuimarisha kazi zake huko Afrika, akisema Umoja wa mataifa utakua mshirika wa kuaminika wa Afrika katika kukabiliana pia na changa moto ya mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo athari zake zitakumba mataifa maskini kabisa katika bara hilo. Alitowa mwito pia wa kushirikiana zaidi kuzuia na kukomesha kabisa mapigano na kuzisaidia nchi zinazo jikokota kutoka vita. Alisema ni kwa kufanya kazi pamoja kwa dhati ndipo tutaweza tanzua matatizo yanayo likabili bara hilo tajiri.

Mnaendelea kuyasikiliza makala ya Mwangaza kutoka radio ya Umoja wa mataifa. Mapema mwezi wa huu, afisi ya Umoja wa Mataifa huko Sudan ilitangaza kwamba, maafisa wa vyeo vya juu wa Umoja wa Mataifa na Jumwia ya Afrika AU, walikutana na makundi ambayo hayakutia sahihi makubaliano ya amani ya Darfur. Lengo la mazungumzo ni kujadili hatua za kuchukuliwa sasa katika utaratibu wa kisiasa ili kumaliza uhasama katika jimbo hilo lenye ghasia huo magharibi ya Sudan. Abdushakur Aboud ana maelezo zaidi.

Kwa muda wa wiki mmoja ujumbe wa pamoja wa upatanishi wa UM na AU ukiongozwa na mjumbe wa UM Pekka Haavisto na Sam Ibok wa AU walikua na mazungumzo na makundi yenye makazi yake huko kaskazini ya Darfur na Asmara, Mji mkuu wa Eritrea.

Makubaliano ya amani yaliyohusu masuala ya usalama, kugawanya utajiri na madaraka yalitiwa sahihi mwezi Mai 2006, kati ya serekali ya Khartoum na sehemu moja ya kundi la ukombozi wa Sudan SLM/A, kwa lengo la kukomesha mapigano makali huko Darfur.

Wakiwa Asmara, wajumbe wa tume walikutana na wakuu wa Eritrea kujadili hatua za kuchukuliwa kusonga mbele katika utaratibu wa amani kama ilivyoelezwa katika mpango ulopendekezwa na mjumbe maalum wa katibu mkuu Ban Ki-moon, Jan Eliasson, unaotoa mwito kwa pande zote kukomesha uhasama na kutayarisha majadiliano yajayo.

Ujumbe huo ulikutana pia na makamu wa kwanza wa Rais wa Sudan Salva Kiir mjini Juba, kusini mwa Sudan na kujadili jukumu la chama chake cha SPLM katika utaratibu wa amani.

Katibu Mkuu Ban amesema kuna fani nne muhimu ambazo Umoja wa Mataifa inakabiliana nayo katika mzozo wa Darfur. Mzozo wa kibinadamu, siasa, kulinda amani na maendeleo.

Katika mkutano na waandishi habari mapema mwezi wa Julai mjini Geneva, alitoa mwito kuimarishwa utaratibu wa amani inayohusisha pia utekelezaji wa makubaliano yaliyo kwisha fikiwa.

Kuhusiana na mpango wa pamoja wa kulinda amani kati ya UM na AU alisema, wananchi wa Darfur wametaabika sana na jumwia ya kimataifa imesubiri kwa muda mrefu. Wakati umefika kuchukua hatua zinazohitajika na ana matumaini kwamba serekali ya Sudan itatekeleza kwa njia njema ahadi zake.

Wakati huo huo Naibu Katibu mkuu Bi Migiro, alitahadharisha kwamba inabidi watu wasisingatiye madai ya wapiganaji tu bali inabidi kuwasikiliza kila mtu huko Darfur. Alisema Mbali na makundi kuna haja ya kuwahusisha wote, anasema kuna makundi ya wanawake na kuna makundi ya kijamii na wote wanalazimika kushiriki katika kupatikana ufumbuzi.

Amesema huu ni utaratibu utakao chukua muda mrefu kidogo, lakini ujumbe huo maalum umetayarisha njia ambayo anadhani ina endelea mbele na UM bila shaka inatowa uungaji mkono wake kamili.