Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bi Migiro apongeza ushirikiano wa AU na UM

Bi Migiro apongeza ushirikiano wa AU na UM

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bi Asha-Rose Migiro, amesifu mafanikio katika ushirikiano mzuri kati ya Jumuia ya Afrika AU na UM katika kupatikana usalama na amani na kuendeleza maendeleo.

Bi Migiro alikua anahutubia mkutano wa viongozi wa AU huko Accra, Ghana, na alitoa mwito wa kuimarishwa ushirikiano huo. Na akizungumza katika mkutano wa kimataifa ya wanawake jana mjini Nairobi, niabu katibu mkuu alitoa mwito wa kuwepo na juhudi kubwa zaidi kukabiliana na athari za HIV na Ukimwi zinazo wakumba zaidi wanawake na wasichana. Alisisistiza haja ya kufanywa mabadiliko kabisa kuyoka ile hali ya kua na miradi na kuingia katika utekelezaji mipango kabambe kwa kuwapa zaidi wanawake na wasichana madaraka na nguvu za kuweza kujiamini.