Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Idadi ya Watu Duniani

Siku ya Idadi ya Watu Duniani

Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon na mkurugenzi mkuu wa Idara ya Idadi ya Watu UNFPA, Bi Thoraya Ahmed Obaid waliadhimisha siku ya Idadi ya Watu, kwa kutoa mwito wa kushirikishwa zaidi wanaume katika afya ya uzazi ili kupunguza idadi ya wanawake wanaofariki kila siku wanapojifungua na kuhakikisha malezi ya usalama. Abdushkaur Aboud ana maelezo zaidi juu ya siku hii. ~~

Kufuatana na takwimu hii leo zaidi ya nusu milioni ya wanawake wanafariki kila mwaka wanapokua wajawazito na kujifungua, asili mia 99 kati ya hao ni katika nchi zinazoendelea.

Katibu mkuu alisema wanawake wengi sana hutabika kutokana na matatizo magumu wakati wa kujifungua ambayo huwenda yaka athiri vibaya kiwango cha maisha ya wanawake na familia zao. Hivyo alisema wanaume wakiwa kama washirika wa afya ya uzazi wanaweza kuokoa maisha ya wengi.Anasema uungaji mkono kutoka bwana anae fahamu vyema uzazi kutaweza kuimarisha matokeo mazuri wakati wa ujauzito na kujifungua wanawake na hiyo inakua ni tofauti kubwa kati ya maisha na kifo wakati wa matatizo ya kiafya inapotokea.

Katika ujumbe wake Bi Obaid alisisitiza kwamba, ujuzi umeonesha kwamba wanaume wanapojihusisha kunaweza kupatikana tofauti kubwa sana wakati inapokuja suala la kuhifadhi afya na maisha ya wanawake na watoto.

Amesema, kila dakika kuna mwanake anae fariki duniani anapojifungua, hivyo alisisitiza, inabidi pasiwepo hata mwanamke mmoja anafariki anapoleta kiumbe kipya.

Tarehe 11 Julai huadhimishwa kila mwaka kama siku ya Idadi ya Watu Duniani kumulika umuhimu wa masuala kuhusiana na wakazi hasa katika maendeleo. Na kwa kuadhimisha siku hii Idara ya Idadi ya Watu ya UM hutoa ripoti ya mwaka na mwaka huu ripoti imeonya kwamba ifikapo mwaka 2030 idadi ya wakazi katika miji itaongezeka kwa marudufu katika nchi za Afrika na Asia kwa kuongezeka watu biliono 1 milioni 700.

Waziri wa mipango na uchumi wa Tanzania Dk. Juma Ngasongwa, amezungumza na sauti ya UM juu ya ripoti hiyo na juhudi nyingine za serekali ya Tanzania kuimarisha maendeleo vijiji katika kujaribu kupunguza watu kuhamia mijini. Akijibu kwanza juu ya tatizo la watu kuhamia mjini alisema.

Juma: Actually katika Afrika tatizo la watu kuhamia mjini ni tatizo la hali ya maisha….

Huyo alikua Dk Juma Ngasongwa waziri wa mipango na uchumi wa Tanzania.Katika nchi zote za dunia, siku ya idadi ya wakazi imesherehekewa kwa mikutano, maandamano na tamasha tofauti kuhamasisha wakazi mwaka huu juu ya umuhimu wa kuwasaidia wanawake katika kipindi cha kuifungua na afya ya uzazi.