Skip to main content

Sudan imekubali furushi la ulinzi wa amani kwa Darfur

Sudan imekubali furushi la ulinzi wa amani kwa Darfur

Serekali ya Sudan wiki hii ilituma barua kwa Baraza la Usalama ilioelezea kukubali kupelekwa katika Darfur helikopta zitakazotumiwa na vikosi vya mseto vya AU na UM katika shughuli za kuimarisha usalama na amani kwa raia wa jimbo la magharibi la Sudan la Darfur.

Maafikiano haya ni miongoni mwa kile kinachojulikana kama "furushi la msaada mzito", wa awamu ya pili, unaohusiana na idhini ya kuipa UM madaraka ya kufadhilia vifaa, zana za kuendesha operesheni za amani pamoja na wafanyakazi wa kimataifa watakaojumuika na vikosi vya AU kwa madhumuni ya kuhakikisha vurugu la Darfur linakomeshwa na raia wanasawazishiwa usalama.

Kwa ripoti kamili sikiliza idhaa ya mtandao.