Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Jipya la Haki za Kiutu laelekea wapi kikazi?

Baraza Jipya la Haki za Kiutu laelekea wapi kikazi?

Hivi karibuni Baraza la Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Kiutu, lenye wajumbe wanachama kutoka Mataifa 47, lilikutana mjini Geneva, Uswiss kwenye kikao chake cha pili, ambapo kulifanyika majadiliano ya wiki tatu mfululizo kusailia mada kadha wa kadha zinazoambatana na taratibu za kuboresha utekelezaji wa haki za kiutu ulimwenguni.

Katika kikao cha awali cha Baraza la Haki za Kiutu kilichokutana mwezi Julai wajumbe wa taasisi hiyo ya kimataifa waliafikiana kutoingiza masuala ya kisiasa kwenye mijadala yao, na pia waliahidi kuwasilisha tamaduni mpya ya kuzilinda na kuzitunza haki za kiutu kwa busara isiyopendelea, na ya kuridhisha, kwa mataifa yote husika.

Sikiliza majadiliano kamili kati ya baadhi ya mataifa wanachama kwenye idhaa ya mtandao.