Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amlilia rais mwendazake Sata

Hayati Rais Michael Sata alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 24 Septemba mwaka 2012. (Picha:UN/Rick Bajornas)

Ban amlilia rais mwendazake Sata

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -moon ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha rais wa Zambia Michael Chilufya Sata kilichotokea October 28 akiwa anapata matibabu mjini London Uingereza.

Taarifa ya Katibu Mkuu kupitia kwa msemaji wake inamnukuu Bwana Ban akitoa rambirambi zake kwa familia ya rasi Sata, serikali na watu wa Zambia  na kuongeza kuwa anakumbuka vyema safari yake nchini humo mwezi February mwaka 2012.

Bwana Ban amesifu nia ya marehemu rais Sata katika kusaidia mahiataji ya maskini nchini Zambia na maono yake katika nchi.

Amesema anatambua historia iliyotukuka ya Zambia katika kuachiana madaraka ya urais kwa kuzingatia katiba ya nchi. Ban amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia Zambia katika juhudi zake za kukuza maendeleo jumuishi uongozi wa kidemokrasia.