Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IRAN wekeni fursa bayana kwa watetezi wa haki za binadamu: Pillay

IRAN wekeni fursa bayana kwa watetezi wa haki za binadamu: Pillay

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesifu hatua yaIranya kuachia huru mapema wiki hi wafungwa 12 wa kisiasa nchini humo huku akiisihi serikali kuchukua hatua murua za kumaliza unyanyasaji dhidi ya watetezi wa haki za binadamu. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi:

(Taarifa ya Jason)

Kati ya wale walioachiliwa ni bi Nasrin Sotoudeh mwanaharakati wa haki za binadamu anayetambulika kimataifa na mshindi wa tuzo la Sakharov la mwaka 2012. Nasrin alikuwa akihudumia kifungo cha miaka sita kutokana na makosa ya kutishia usalama wa taifa. Rupert Colvile ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva.