Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa tajiri yaondoa vikwazo katika uwekezaji

Mataifa tajiri yaondoa vikwazo katika uwekezaji

Imebainika kuwa mataifa tajiri zaidi kiuchumi duniani pamoja na yale yanayoinukia kiuchumi ya G20 yanaendelea kutimiza ahadi zao za kuondoa vuzuizi kwenye uwekezaji baada ya mataifa hayo kushuhudia hali mbaya ya kiuchumi.

Kulingana na ripoti kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la biahara na maendeleo UNCTAD pamoja na shirika la ushirikiano wa kiuchumu na maendeleo OEDC ni kuwa nyingi ya hatua zilizochukuliwa na mataifa ya G20 kuanzia mwezi Oktoba mwaka uliopita ziliondoa vizuizi kwenye uwekezaji wa kimataifa au kuwahakikisha mema wawekezaji wa kigeni.

Hata hivyo ripoti hiyo inaonyesha kuwa kwa muda wa miezi sita iliyopita kumeongezeka hatua za kudhibiti uwekezaji wa kigeni.