Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 AGOSTI 2024

23 AGOSTI 2024

Pakua

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika ripoti ya kuthibitishwa kwa mgonjwa wa polio huko Gaza; Tukio la uzinduzi wa mpango wa utoaji taarifa mapema kuhusu majanga; Makala ikimulika kazi za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC na mashinani ikienda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mhudumu wa afya anayefanikisha kazi za uteguaji wa mabomu yaliyotegwa ardhini.

  1. Vuta nikuvute ikiendelea Gaza kuhusu ufikishaji, usambazaji na utoaji wa chanjo dhidi ya polio wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima kutoka jeshi la Israeli, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, limethibitisha kubainika kwa mgonjwa mmoja wa polio, ikiwa ni miaka 25 tangu ugonjwa huo utokomezwe eneo hilo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
  2. Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amezindua mpango wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtu anapata Maonyo ya Mapema kuhusu hali ya hewa, EW4All ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027 huku akitangaza uwekezaji mpya muhimu ili kuboresha uchunguzi wa kimsingi wa hali ya hewa, uzinduzi uliofanyika katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.
  3. Makala inasalia makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ikiwa leo ni siku ya mwisho ya maonesho ya picha yaliyoandaliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Anold Kayanda anatupitisha katika picha hizo zinazoonesha athari mbalimbali kwa wanadamu kutokana na uhalifu unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani. Kwako Anold
  4. Mashinani: Fursa ni ya Chantal Zingapako, muuguzi anayejitolea kusaidia timu ya  ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, ya kutegua mabomu ya ardhini.
Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
10'19"