Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Operesheni ya ukozi inaendelea Ethiopia kufuatia maporomoko ya udongo: OCHA

Mama wa watoto watano akipokea msaada wa chakula katika eneo la eneo katika eneo la Oromia, Ethiopia. (Maktaba)
© WFP/Michael Tewelde
Mama wa watoto watano akipokea msaada wa chakula katika eneo la eneo katika eneo la Oromia, Ethiopia. (Maktaba)

Operesheni ya ukozi inaendelea Ethiopia kufuatia maporomoko ya udongo: OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura  OCHA limesema operesheni ya kusaka na kuokoa waliofunikwa katika maporomoko ya udongo Kusini mwa Ethiopia inaendelea.

Katika maporomoko hayo yaliyochochewa na mvua kubwa  duru za habari zinasema  zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha lakini mamla ya nchi hiyo imeyaambia mashirika ya Umoja wa Mataifa kuwa takriban watu 157 wamekufa katika jimbo hla Kusini mwa Ethiopia na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka  .

OCHA inasema zaidi ya watu 14,000 wameathirika na maporomoko hayo.

Msaada kwa waathirika

Mamlaka zajimbo hilo na Shirika la chama cha Msalaba Mwekundu la Ethiopia tayari wametuma misaada ya awali katika eneo hilo.

OCHA inaratibu tathmini ya kibinadamu na leo mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na la kuhudumia watoto  UNICEF, la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Shirika la Afya Duniani WHO na la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA yanalenga kusambaza vifaa muhimu, ikiwa ni pamoja na chakula, vifaa vya matibabu na msaada wa maji, usafi wa mazingira na usafi.

Tathmini hiyo itasaidia kujua kiwango cha watu waliotawanywana maporomoko hayo na uharibifu unaosababishwa na mvua zinazoendelea na maporomoko hayo ya udongo.

Hivi sasa, mahitaji muhimu zaidi kwa wale walioathiriwa ni chakula, malazi, huduma za afya, na maji, usafi wa mazingira na usafi.