Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji Samburu: Ngamia sio tu wamenusuru familia zetu, pia wametufungulia ukurasa mpya

Wafugaji Samburu: Ngamia sio tu wamenusuru familia zetu, pia wametufungulia ukurasa mpya

Pakua

Kauti ya Samburu Kaskazini mwa Keny ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ya Wasamburu kwa kawaida ni wafugaji, baada ya ukame kukatili maisha ya mifugo yao haswa ng’ombe na mbuzi wakazi wengi walipoteza matumaini hadi pale FAO ilipowaletea mradi wa ufugaji wa ngamia kama mbadala wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. 

Nankaya Lepitiling, mwanachama wa kikundi cha wanawake cha Salato Samburu ambaye ameona faida ya ufugaji wa ngamia kupitia mradi wa FAO, anasema “Tumewaonna ngamia kwa mda mrefu kwenye kikundi chetu, na mimi niimeshakuwa kiongozi wa kikundi cha Salato, tulipewa ngamia wa mradi, wanafika karibu  ngamia 30 hivi”

Ntomuan Selaina naye ni mnufaifa wa mradi huo..

“Wametusaidia  sana kwa chakula cha  watoto, hakuna shida hata kidogo, hata chai wengine wanakunywa ya siturungi nami nakunywa ya maziwa , nawapatia pia watu wengine na sasa kuna huyu mtoto  amekuja hapa kwa sababu mama yake hana maziwa tunampatia ya ngamia wngu.”

Kwamujibu wa FAO ukame ulichochea ongezeko la utapiamlo na magonjwa mengine ya ukosefu wa lishe bora hususan miongoni mwa  watoto ndio FAO ikachukua hatua kwa kuanza kugawa ngamia kupitia mradi wa ubunifu wa PEAR ambao pia unawapa wafugaji mafunzo . Timothy Lesingran ni mtaalam wa wanyama katika mradi huo wa PEAR

“Tunatoa mafunzo kwa wanawake na tumewafunza wanawake wengi tuu katika ngazi mbalimbali na wengi wamefurahia sana kufanyakazi nasi.”

Pia mradi huu umewapa wanawake hawa wafugaji fursa nyingine kama wanavyosema Ntomuan na Nangaya,

“Hata vikapu tunavyotumia kukamua maziwa tunavishona wenyewe na tunaviuza pesa tunayopata tunanunua chakula cha kutulisha sisi na watoto wetu. Na tangu tulipopata ngamia tena tukenda kujenga mahali pengine duka la maziwa sasa tunakamua maziwa , tunayaweka kwenye mashine, tunachuja mafuta , tunauza maziwa freshi na mazia lala, na tunatengeneza peremende ya jibini ya maziwa ya ngamia”

Mradi huu wa FAO umewalenga zaidi wanawake na familia zinazogawiwa ngamia zimewajibika kutia saini mkabata unaosema ngamia waliyepokea ni wa mama wa familia hiyo, lakini faida kubwa imekuwa kwa familia  nzima na hasa watoto kama Juma Lesaina mtoto wa Ntomuan, anasema mama (PARAPHRASE)“Alininunulia sare za shule kutokna na maziwa aliyopata ya ngamia na  ndipo nilipoweza kujiunga na shule kwa msaada wa ngamia, na nimesomea uhandisi wa masualaya umeme , hivyo nimefika hapa nimatokeo ya ngamia na watu waliona ngamia maisha yao yamebadilika.”

FAO sasa imepanua wigo wa mradi huo katika kaunti zingine za jirani ikiwemo Isiolo na lengo ni kuzifikia kaunti nyingi zaidi za wafugaji.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Selina Jerobon
Audio Duration
3'9"
Photo Credit
UN News/Thelma Mwadzaya