Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu UN azindua maono mapya ya amani katika 'ulimwengu wenye mataifa mengi yenye nguvu'

Bendera za mataifa mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa zikipepea nje ya makao makuu ya umoja huo jijini New York Marekani
UN Photo/Rick Bajornas
Bendera za mataifa mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa zikipepea nje ya makao makuu ya umoja huo jijini New York Marekani

Katibu Mkuu UN azindua maono mapya ya amani katika 'ulimwengu wenye mataifa mengi yenye nguvu'

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amewasilisha Tamko jipya la Kisera kuhusu Ajenda Mpya ya Amani, ambayo inaelezea maono yake ya juhudi za kimataifa za amani na usalama, kwa kuzingatia sheria za kimataifa. 

Akihutubia Nchi Wanachama lwa Umoja wa Mataifa leo Alhamisi (20 Julai), Guterres amesema, "Tuko kwenye hatihati ya enzi mpya. Kipindi cha baada ya Vita Baridi kimekwisha, na tunaelekea kwenye mpangilio mpya wa kimataifa na ulimwengu wa nchi zenye nguvu sawa. Tamko hili la kisera kuhusu Ajenda Mpya ya Amani linaeleza maono yangu ya juhudi za kimataifa kwa ajili ya amani na usalama, kwa kuzingatia sheria za kimataifa, kwa ulimwengu katika kipindi cha mpito. 

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, "zama hizi mpya tayari zimetiwa alama na kiwango cha juu zaidi cha mivutano ya kijiografia na ushindani mkubwa wa madaraka katika miongo kadhaa."  

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kusema, “Ukiukaji wa sheria za kimataifa unazidi kuwa wa kawaida. Malalamiko ya kina na, katika baadhi ya matukio, kuhusu viwango viwili na ahadi ambazo hazijatimizwa yanadhoofisha ushirikiano. 

Wakati huo huo, ameendelea Guterres kwamba, "ulimwengu unakabiliwa na vitisho vipya na vinavyositawi ambavyo vinahitaji hatua za haraka na za umoja." 

Katibu Mkuu amesema"migogoro imekuwa migumu zaidi, mbaya zaidi, na ngumu zaidi kusuluhisha" na akabainisha kuwa mwaka jana kulikuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo vinavyotokana na migogoro katika karibu miongo mitatu. 

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia amekumuska kwamba "wasiwasi juu ya uwezekano wa vita vya nyuklia umeibuka tena" na "maeneo mapya ya migogoro na silaha za vita yanaunda njia mpya ambazo ubinadamu unaweza kujiangamiza." 

Guterres ameongeza kusema, “Tamko la kisera kuhusu Ajenda Mpya ya Amani linaeleza mapendekezo mengi na madhubuti ambayo yanatambua hali ya uhusiano kati ya nyingi za changamoto hizi. Imeandaliwa kulingana na kanuni za msingi za uaminifu, mshikamano, na ulimwengu wote ambazo ni msingi wa Mkataba na kwa ulimwengu thabiti. 

Kwa Katibu Mkuu, "amani ndiyo nguvu inayosukuma kazi ya Umoja wa Mataifa" na "matishio mapya ya amani yanaleta matakwa mapya kwetu." 

Ameongeza, “Muhtasari huu wa Sera ni jaribio letu la kukidhi matakwa hayo. Ninaomba Nchi Wanachama kujadili Ajenda Mpya ya Amani na kujihusisha na mapendekezo yetu. 

Guterres amesema kuwa Umoja wa Mataifa "ni, na lazima ubaki, kitovu cha ushirikiano wa kimataifa."