Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Imetosha damu inayomwagika kwa ugaidi Somalia:UNSOM

Vikosi vya usalama vya jeshi la Somalia na vile vya Muungano wa Afrika AMISOM vikiwa katika msafara kuelekea Barawe ambako ni ngine imara ya Al-Shbaab.
Picha na AMISOM/Tobin Jones
Vikosi vya usalama vya jeshi la Somalia na vile vya Muungano wa Afrika AMISOM vikiwa katika msafara kuelekea Barawe ambako ni ngine imara ya Al-Shbaab.

Imetosha damu inayomwagika kwa ugaidi Somalia:UNSOM

Amani na Usalama

Shambulio la kigaiodi mjini Gaalikacyo Somalia limekatili maisha ya watu watano wakiwemo maafisa usalama wa serikali na raia waliokuwa wamefurika kwenye mgahawa mmoja mjini humo.

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM umelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea leo Katikati mwa Somalia kama jaribio la kutaka kusambarataisha mchakato wa upatanisho.
    
Kwa mujibu wa UNSOM shambulio hilo limetokea kwenye mhgahawa uliokuwa umefurika watu wengi mjini Gaalkacyo na kukatili maisha ya watu watano wakiwemo maafisa usalama wawili wa serikali na raia , huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. 


Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ambaye pia ni mkuu wa UNSOM , Michael Keating amesema shambulio hilo limetokea kwa sababu wafuasi wa itikadi kali wanatiwa hofu na hatua zilizopigwa katika juhudi za upatanishi mjini Gaalkacyo.


Ameongeza kuwa taifa hilo “limeteseka vya kutosha na machafuko na umwagaji damu na sasa ni wakati wa upatanisho.”


Taarifa za awali zinasema mshambuliaji wa kujitoa muhanga alijilipua katika mtaa wa Jiiro Abdullahi Yusuf, ambako vikosi vya usalama vilikuwepo na, Kundi la kigaidi la Al-Shabaab limeripotiwa kudai kuhusika na shambulio hilo.


UNSOM imetuma salamu za rambirambi kwa familia na waliokuwa wakifanya kazi na wahanga wa shambulio hilo huku wakiwatakia afueni ya haraka majeruhi.