Mbali ya adha, ukosefu wa maji huchagiza pia migogoro- UNAMID
Hali ya upatikanaji wa rasilimali ya maji kwa maelfu ya wakazi wa jimboni Darfur nchini Sudan ni mtihani mkubwa unaochangia pia kuendelea kwa migogoro.
Hayo yamesemwa leo na Olatunji Ayeni, mkuu wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur, UNAMID anayehusika na idara ya ulinzi wa amaji na mazingira, akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa wimbi kubwa la watu wanaohama maeneo mengine na kuingia Darfur, na hali ya ukame vimezidisha adha ya kupata rasilimali hiyo muhimu.
(Sauti ya Olatunji Ayeni)
“Hali ya upatikanaji wa maji safi Darfur ni mbaya hasa kwa upande wa maji ya kunywa, ukiangalia kwa upande wa rasilimali, hili ni moja ya eneo lenye hali mbaya sana ya hewa duniani, halina vyanzo vya rasilimali ya maji, halina mito, hivyo bado ni changamoto.”
Na kuhusu ongezeko la watu na migogoro amesema
(Sauti ya Olatunji Ayeni)
“Ongezeko la idadi ya watu hivi karibuni imeongeza changamoto kubwa katika rasilimali ya maji ambayo tayari ilikuwa adimu na ni vigumu kuiongeza, wanawake na wasicha ambao wangepaswa kuwa shule wanatumia sehemu kubwa ya maisha yao kwenda mbali kusaka maji. Ukiangalia kiukweli ni kwamba kiasili maji yamebainika kuwa ni moja ya sabau zisizo za kisiasa zinazochochea migogoro."