25 JUNI 2024
Pakua
- Katika Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati tathmini mpya iliyofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani WFP imethibitisha wasiwasi wa kuendelea kuwepo kwa viwango vya njaa ambapo asilimia 96 ya wananchi wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
- Leo ni siku ya mabaharia duniani ikibeba maudhui ya kuangalia usalama wao kazini. Katika ujumbe wake kwa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kukomeshwa kwa vitendo vya kiharamia vya meli kutekwa nyara na kueleza kuwa mabaharia hawapaswi kuwa waathiriwa wa migogoro ya kijiografia na kisiasa.
- Na ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO imeonesha vifo milioni 2.6 kwa mwaka vinachangiwa na unywaji pombe hii ikiwa ni sawa na asilimia 4.7 ya vifo vyote duniani, na vifo laki sita kwa matumizi ya dawa za kulevya.
- Mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabaharia, na kupitia ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya baharí, IMO Arsenio Dominguez anawatakia kila la heri mabaharia wote akiwaalika katika meza ya kubonga bongo kuhusu masuala ya usalama wa baharini.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
9'53"