Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 MEI 2024

20 MEI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya sheria na uhalifu na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini CAR kufatilia kazi za walinda amani na mashinani tunakuletea ukumbe kuhusu ufugaji nyuki na thamana yao. 

  1. Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. 
  2. Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.
  3. Makala inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto.
  4. Na katika mashinani leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Nyuki tutasikia uhusiano kati ya nyuki na  jamii za watu wa asili.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
11'20"