Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Gaza waamua vita isiwe sababu ya kunyong’onyea wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Watoto Gaza waamua vita isiwe sababu ya kunyong’onyea wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Pakua

Huko Ukanda wa Gaza, vita inayoendelea tangu Oktoba 7 mwaka 2023 baada ya Hamas kurusha makombora Israel na kisha Israel kuamua kujibu mashambulizi licha ya kusababisha vifo vya watu 31,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto, watoto waliosalia wameona mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani usipite hivi hivi. Wakiwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Deir El Balah katikati mwa Gaza, watoto hao wameona furaha ni bora kuliko machungu ya njaa, ukimbizi, ukosefu wa huduma muhimu za kijamii unaowakabili. Mwandishi wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa huko Gaza, Ziad Talib amefika hapo ili kufahamu hasa msingi wa hatua ya watoto hao na ndio makala ya leo inayosimuliwa na Assumpta Massoi.

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'35"
Photo Credit
UN News/Ziad Taleb