Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 DESEMBA 2024

13 DESEMBA 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo leo ulimwengu unaadhimisha Siku ya kimataifa ya redio duniani, dhima ya mwaka huu ikiwa 'Karne katika kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha'. Pia tunakuletea habari kwa ufupi. Mashinani tunasalia na maadhimisho ya siku redio.

  1. Leo ni siku ya Radio duniani na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa karne moja chombo hicho lkimekuwa kikihabarisha, kuburudisha na kuelimisha jamii kote duniani. Mwaka huu siku hii inaenzi utajiri uliuopita wa Radio, kuendelea kwa umuhimu wake na matarajio ya mustakbali wake ingawa kinaendelea kukabiliwa na changamoto hasa kutoka kwenye majukwaa ya kidijitali na changamoto za kiuchumi. Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay katika ujumbe wake amesema “Katika siku hii ya Radio, tunasherehekea sio tu historia ya Radio lakini pia jukumu lake muhimu katika jamii zetu sasa na miaka mingi ijayo.”
  2. Gaza, Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini akizungumza na nchi wanachama hii leo amewaomba waliokata ufadhili kwa shirika hilo “Kubadili maamuzi yao hususan kwa mtazamo kwamba wafanyakazi waliodaiwa kushiriki uhalifu walifutwa kazi mara moja na uchunguzi unaendelea.” 
  3. Namalizia na Sudan ambako kaimu mwakilishi wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO nchini humo Peter Graaff, akizungumza mjini Cairo Misri hii leo kuhusu hali ya Sudan amesema miezi kumi ya vita imetumbukiza mamilioni ya watu katika janga lisiloelezeka la kibinadamu huku mapigano yakiendelea kusambaa katika maeneo mapya na kufurusha watu zaidi wengine mara kadhaa.
  4. Na katika mashinani tunakutana na mkaazi wa Karen Nairobi nchini Kenya ambaye anasema kupitia matangazo na vipindi vya redio hutaachwa nyuma wakati fursa za biashara au nafasi za ajira zinavyotokea.    

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'32"