Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakikisha usalama zaidi ili wahudumu wa kibinadamu waweze kusambaza chakula Sudan - WFP

Hakikisha usalama zaidi ili wahudumu wa kibinadamu waweze kusambaza chakula Sudan - WFP

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limezitaka pande zinazohasimiana nchini Sudan kutoa hakikisho zaidi la usalama kwa shirika hilo ili liweze kusambaza msaada wa chakula kwa wananchi waliokimbia makazi yao na waliokwama katikati ya mapigano ili kuwanusuru watu hao kutokufa njaa. 

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao huko Geneva Uswisi, Msemaji wa WFP nchini Sudan, Leonie Kinsley amesema hali ya chakula nchini humo ni mbaya sana, licha ya juhudi zinazofanywa na shirika lao kutoa Msaada kwa watu milioni 6.5,  bado watu milioni 18 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Kinsley amesema “WFP kwa sasa ina uwezo wa kutoa msaada wa haraka wa chakula kwa mtu mmoja kati ya 10 ambao wanakabiliwa na hali ya dharura ya njaa nchini Sudan. Ikimaanisha asilimia 90 ya watu ambao ni wenye njaa zaidi hawapati msaada.”

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Khartoum, Darfur and Kordofan na sasa jimbo la Jazeera, ambako mzozo ulisambaa mwezi Desemba mwaka jana.

WFP imeeleza kuwa chakula kipo nchini humo lakini inawawia vigumu kukisambaza na wanakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo kuporwa kwa chakula katika ghala lao la chakula huko jimboni Jazeera.

“Ili Msaada uweze kuwafikia wananchi, misafara ya misaada ya kibinadamu lazima iruhusiwe kuvuka katika eneo lenye mapigano. Hata hivyo imekuwa vigumu hilo kufanyika kutokana na vitisho vya usalama, mapigano yanayoendelea na kulazimishwa kuwekewa vizuizi barabarani wakidai ada na ushuru. Hali nchini Sudan leo ni janga. Mamilioni ya watu wameathiriwa na mzozo huo.”

Angalau juhudi za WFP kusaka hakikisho la usalama ili kusambaza chakula zimezaa matunda wiki iliyopita, na sasa usambazaji wa misaada unaendelea huko Kassala, Gadhafi na jimbo la Blue Nile.

Hata hivyo malori mengine 31 ya WFP, ambayo yalipaswa kupeleka misaada ya mara kwa mara huko Kordofan na White Madani, yameegeshwa tupu yakishindwa kuondoka.

Hata hivyo malori mengine 31 ya WFP, ambayo yalipaswa kupeleka misaada ya mara kwa mara huko Kordofan na White Madani, yameegeshwa tupu yakishindwa kuondoka. 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
2'14"
Photo Credit
© WFP/Eloge Mbaihondoum