Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanafunzi Msumbiji: Iwe mvua iwe upepo mkali madarasa yetu ni salama

Mwanafunzi Msumbiji: Iwe mvua iwe upepo mkali madarasa yetu ni salama

Pakua

Kila mwaka, Msumbiji hukabiliwa na matukio ya hali mbaya za hewa kupindukia kama vile vimbunga na mafuriko, matukio ambayo husababisha uharibifu wa shule na hatimaye watoto kushindwa kujifunza. Hata hivyo, ujenzi wa madarasa yanayohimili matukio kama vile pepo kali na mafuriko umeleta nuru na matumiani kwa watoto, wazazi na walimu. Madarasa haya yanawezesha watoto kubakia salama hata wakati wa mvua na upepo mkali. Hali hii ni uwekezaji wa kudumu kwani ni  hakikisho kwa watoto kuendelea kupata elimu na mustakabali wao kuwa bora. Selina Jerobon wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anamulika ni kwa vipi hilo limefanyika kupitia mradi uliofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Audio Credit
Flora Nducha/Selina Jerobon
Sauti
4'11"
Photo Credit
UN Habitat Mozambique