Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakazi wa Ituri, DRC, wazungumzia usaidizi wa MONUSCO kwenye eneo lao

Wakazi wa Ituri, DRC, wazungumzia usaidizi wa MONUSCO kwenye eneo lao

Pakua

Katika jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, watu waliokimbia makazi yao wanaishi katika takribani kambi 38, ambapo miongoni mwao ni Drodro, Roe, Lodha, Jaiba na Gina. Zaidi ya wakimbizi Laki Nne (400,000) wanafaidika na ulinzi wa moja kwa moja wa ujumbe wa walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.  Walinda amani hao wakiwemo wale wa kutoka Nepal hulinda kambi za watu waliohamishwa kwa kufanya doria za usiku na mchana. Na zaidi ya yote MONUSCO imeweka miundombinu ya kuhakikishia raia usalama wao, moja ya majukumu ya ujumbe huo ambao kwa sasa unaanza kufunga virago taratibu kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia ombi la serikali ya DRC. Katika makla hii mwandishi wetu wa habari mashariki mwa DRC George Musubao alifuatilia mtazamo wa wananchi kuhusu usaidizi wa MONUSCO

  

Audio Credit
Leah Mushi/George Musubao
Audio Duration
4'24"
Photo Credit
UN News