Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Botswana wako mstari wa mbele kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Botswana wako mstari wa mbele kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Pakua

Botswana iko njiani kutokomeza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI - VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, shukrani kwa msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO kanda ya Afrika wakishirikiana na mashirika ya kiraia. 

Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. 

Botswana ni moja ya nchi zinazokuwa na changamoto ya maambukizi ya VVU, mwaka 2022 wizara ya afya ya Botwasana wakishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika na mashirika ya kiraia waliunganisha nguvu kushughulikia changamoto hiyo ambayo ilikuwa ikiwaathiri wajawazito wanaoishi na VVU kwani walikuwa hawajui mengi kuhusu haki zao ikiwemo haki ya faragha, usiri na ruhusa ya kutoa taarifa zao.

WHO na wadau wengine walitoa mafunzo kwa wawakilishi 27 wa vikundi vya msaada kwa watu wanaoishi na VVU, wahudumu wa afya katika ngazi ya jamii na watu waliojitolea, na wote hawa walipewa jukumu la kuelimisha wenzao juu ya haki za binadamu, kutoa ridhaa baada ya kuarifiwa na usawa wa kijinsia kama anavyoeleza Layeza Maraya Mbulawa, Muuguzi mkuu katika Kliniki ya Thini iliyoko Tutuma nchini Botswana. 

Tumepewa mafunzo ya haki za binadamu, ambayo tunayatekeleza katika ngazi ya wilaya ambapo safari hii kuna mabadiliko makubwa. Watu wanajua haki ya binadamu.”

Na sasa wanawake wanaoishi na VVU wanajua zaidi kuhusu haki zao hususan kwenye masuala ya afya kama anavyoeleza mmoja wa wanufaika ambaye jina lake hatutalitaja. 

“Siku hizi mambo yamekuwa bora sana kwa sababu sasa najua kuhusu haki zangu na hakuna anayefanya maamuzi kwa niaba yangu na mtu unaweza kuamua unachotaka.”

Kuimarisha haki ya afya ni kusaidia kuimarisha huduma bora. Afya kwa wote ni kitovu cha mapambano dhidi ya VVU nchini Bostwana.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
2'1"
Photo Credit
@Donald Bliss/NLM/NIH