Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani kutoka Tanzania watoa mafunzo ya mapishi na ujasiriamali kwa wanawake wanakijiji cha Moro, CAR

Walinda amani kutoka Tanzania watoa mafunzo ya mapishi na ujasiriamali kwa wanawake wanakijiji cha Moro, CAR

Pakua

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR (MINUSCA) wametoa mafunzo ya upishi kwa vikundi vya wanawake wa Kijiji cha Moro kilichoko takribani kilometa 50 kutoka Mji wa Berberati, jimboni Mambere Kadei yalipo makao makuu ya kikosi hicho.  

Wakiwa na shangwe na nderemo wanakijiji cha Moro wanawapokea walinda amani kutoka Tanzania chini ya MINUSCA katika Kijiji hicho...Kisha walinda amani hao wanaanza kutoa elimu ya mapishi kwa vitendo kwa wanawake ili kuwapa njia ya kujipatia kipato na lishe kupitia utengenezaji wa vitafunwa kama vile mandazi. Wanawake wameona kuanzia jinsi ya kuchanganya unga, kukoroga, kuumua hadi mwisho kupata 

Chifu wa Kijiji cha Moro Jack Bambakyr anatoa shukrani zake kwa TANBAT6  kwa elimu waliyotoa akisema, "Ninatoka shukrani kwa walinda amani kutoka Tanzania kwa sababu ya mambo mapya ambayo wamekuja kuwaonesha wake zetu hapa. Wamepata ujuzi wa kutengeneza vitu mbalimbali kwa mikono Ili kujipatia kipato.  Asante sana, asante sana kwa kuja kwetu." 

Naye Mwenyekiti wa vikindi vya ujasiliamali vya wanawake wa kijiji Cha Moro Bi. Marie Aghateanatoa shukrani zake kwa TANBAT6 huku akiwasihi wapatapo nafasi warudi tena kuwapatia elimu zaidi, "Kwa niamba ya kinamama nashukuru sana Kwa  kutupa uelewa zaidi wa kujipatia kipato. Asanteni watanzania tunaomba mnapopata nafasi msisite kuja tena Kijiji hapa"

Sasa ni matunda ya kile walichofundishwa  wanakijiji, wanakula na kunywa uji na mandazi. 

Audio Credit
Kapteni Inyoma
Audio Duration
2'11"
Photo Credit
TANBAT 6/Kapteni Inyoma