Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mariam: Dawa za kulevya zilinifanya kupoteza mtoto na mume

Mariam: Dawa za kulevya zilinifanya kupoteza mtoto na mume

Pakua

Tatizo la dawa za kulevya duniani ni suala tata ambalo linaathiri mamilioni ya watu duniani kote. Watu wengi wanaotumia dawa za kulevya hukumbana na unyanyapaa na ubaguzi, jambo ambalo linaweza kudhuru zaidi afya yao ya kimwili na kiakili na kuwazuia kupata usaidizi wanaohitaji.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu UNODC inatambua umuhimu wa kuchukua mtazamo unaozingatia watu kuhusu sera za dawa za kulevya, kwa kuzingatia haki za binadamu, huruma na mazoea yanayotegemea ushahidi. 

Miongoni mwa shuhuda nzuri katika jamii ni kuwa wale waliotumia dawa za kulevya wanaweza kurejea kwenye afya zao na maisha yao ya awali iwapo wataacha na kukaaa kwenye vituo vya matibabu ya uraibu na matibabu. Mariam, sio jina lake halisi alikubali na kukaa kituoni na hii ni simulizi yake iliyoandaliwa na UNODC na inasomwa kwako na Evarist Mapesa wa redio washirika SAUTFM iliyoko Mwanza nchini Tanzania.  

Audio Credit
Selina Jerobon/Evarist Mapesa
Sauti
4'1"
Photo Credit
UNAMA / Eric Kanalstein