Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 APRILI 2023

25 APRILI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikimulika Malaria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo tarifa ya WHO ya siku ya malaria duniani, wakimbizi wa Sudan na ripoti mpya ya FAO. Mashinani tunakuletea ujube kuhusu maambukizi ya malaria.

  1. Leo ni siku ya malaria duniani mwaka huu ikibeba kmaudhui “Wakati wa kutokomeza kabisa malaria:Kuwekeza kubuni na kutekeleza”. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataoifa duniani WHO mwaka huu linajikita zaidi katika utekelezaji na hasa umuhimu wa kuwafikiwa watu walio hatarini Zaidi  kwa mikakati na nyenzo zilizopo ili kutokomeza ugonjwa huo unaokatili Maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka.
  2. Shirika la Umoja wa Matyaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema linaongeza jitihada kuwasaidia maelfu ya watu wanaokwenda kusaka usalama katika nchi za jirani na Sudan wakikimbia nchini mwao ambayo yanaonekana kuendelea kutawanya watu ndani na nje ya nchi.
  3. Na nyama, mayai na maziwa vimeelezwa katika ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kuwa ni chanzo muhimu cha vitutubisho vinavyohitajika mwili ambavyo haviwezi kupatikana kwa urahisi katika lishe itokanayo na mimea.
  4. Mashinani na tutakuletea ujumbe kuhusu usugu wa vimelea vya malaria na njia za kuudhibiti

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'22"